Tatizo kubwa la kuwepo kwa rushwa sana katika mkoa wa shinyanga linatokana na mambo makuu kama ifuatavyo:-
1.Elimu ndogo kwa wananchi kuhusu haki zao za msingi na jinsi ya kuzipata.
Tatizo la elimu ya kujua kusoma na kuandika kusikia na kuongea kiswahili linaongoza kuwafanya wenyeji hawa hata mahali panapotolewa huduma kama kiliniki ya hakina mama wajawazito na watoto kulipiwa pamoja na matangazo yaliyobandikwa mahali hapo kuwa huduma hizo ni bure. Hapa ni mhudumu wa kiliniki kuitangaza kuwa kila kadi itakayotolewa iambatane na shilingi mia vinginevyo huduma hupati.
Jambo lingine ni uwezo wa kuhoji kwa msukuma kuambiwa na mtendaji au polisi ku wa uko chini ya ulinzi kwa tuhumala kushirki mauaji ya kikongwe au kwa kuhudhuria mwano wa sungusungu uliosababisha mauaji. Hapo polisi/mtendaji anataja hukumu kuwa kosa hili ni miaka 30 kwa msukuma hiyo ni hukumu tayari. Jamii yote inaamini kuwa tayari kaishafungwa.
Nitatoa mifano kidogo, kwa msukuma neno dhamana ya polisi au mahakama ni pesa taslim ni fedha nyingi laki hadi millioni kadhaa.
2. Kuwepo kwa uwezo mkubwa wa uchumi hasa mifugo na mavuno ya pamba n.k
Kuwepo kwa mifugo kama chanzo kikubwa cha uchumi kwa msukuma ni rahisi kutoa fedha au mifugo kwa hakimu ,polisi n.k kwa imani kuwa atasidiwa kuepuka hukumu au kosa lako kielelezo ni kuwepo kwa mahakimu wa ngazi zote za mkoa huu wenye utajiri wa mali na mifugo.
Kwa msukuma ni jadi kutamba kuwa baskeli yake ni phonex ya tsh 80,000.00 mwenzake anenda dukani kununua baiskeli hiyo kwa Tsh 100,000.00 na kuhakikisha amepata stakabadhi ya fedha hiyo aje atambe.
3.Mila na desturi za kisukuma kuhusu mahari na imani za kishirikiana
Kwa msukuma mtoto wa kike ni mtaji yaani utajiri kupitia mahari kati ng'ombe 20-40 , kwa hali hiyo kwa nini msichana asitoroshwe shule akaolewe na mzee tajiri . Mwalimu au mtendaji akifuatilia anapewa ng'ombe 2, kesi ikipelekwa poliasi mpelelezi ng'ombe 2, mahakamani hakimu ng'ombe 2. Shauri limekwisha.
4. Watumishi wa vyombo kama polisi , viongozi/watawala(W.E.O & V.E. O) na mahakama kutofuata sheria, kanunu na taratibu katika kutoa huduma.
Watumishi wanatoa huduma katika sehemu hizi wamesahau kabisa kanuni na maadili ya kazi zao si kwa kuwa hawazifahamu bali ni jinsi ya kuongeza mapato yao, vilvile kukwepa vyombo vinavyofuatilia tuhuma za rushwa vikose ushahidi unaotegeme sheria ,kanuni na taratibu.
Kwa mkoa huu polisi anaweza kwenda kufanya upekuzi kwa mwananchi bila hati ya upekuzi wala shahidi wa upekuzi saa kumi usiku na bila kutumwa na kiongozi wake wa kazi. Mtendaji wa kata au kijiji anaweza kumweka ndani mtu anayedaiwa deni la jirani yake kwa siku 5.
![]() | |
| BACK | |
| |
|