Kama hali imekuwa mbaya kama anavyosimulia Ummy ni kwamba Tanzania inarudi nyuma katika wakati wa UKOLONI. Sisi ambao tulipata fursa ya kuona kidogo wakati huo tunakumbuka kwamba wazalendo tulikuwa ni “mtu wa tatu”.Kwanza alihudumiwa Mzungu halafu Mhindi na halafu “mtu wa tatu”.
Lakini sasa hawa wahindi ni watanzania ndugu zetu. Wengi wao wanasema tu kuwa ni wahindi lakini huko India hana ndugu hata mmoja bali ndugu zake ni sisi. Wengi wao baba au babu zao walikuja Tanganyika mwaka 1906 na hawakurudi tena India baada ya kujenga reli kati ya Tanga-Moshi-Arusha na ile reli ya Dar es Salaam –Tabora-Kigoma.
Ubaguzi unaofanywa na hao watowaji huduma kwa ajili ya fedha za rushwa ni mbaya sana kisiasa. Unaweza kuleta vurugu katika nchi.
Kuna watu wanodhani kwamba sisi watu “weusi” tumelaadiwa.Tukienda Ulaya tnabaguliwa,tukienda Amerika tunabaguliwa, tukienda India tunabaguliwa,tukienda Autralia tunabaguliwa.Lakini hata sisi wenywe kwa wenyewe Tanzania tunabaguwana kwa ajili ya umasikini wetu na roho mbaya.
Hakuna mtu yeyote ambaye ametulaani.
![]() | |
| BACK | |
| |
|